Psalms 136

Wimbo Wa Kumshukuru Mungu


1 aMshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.

Fadhili zake zadumu milele.

2 bMshukuruni Mungu wa miungu.

Fadhili zake zadumu milele.

3 cMshukuruni Bwana wa mabwana:

Fadhili zake zadumu milele.


4 dKwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,

Fadhili zake zadumu milele.

5 eAmbaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,

Fadhili zake zadumu milele.

6 fAmbaye aliitandaza dunia juu ya maji,

Fadhili zake zadumu milele.

7 gAmbaye aliumba mianga mikubwa,

Fadhili zake zadumu milele.

8 hJua litawale mchana,

Fadhili zake zadumu milele.

9 Mwezi na nyota vitawale usiku,

Fadhili zake zadumu milele.


10 iKwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

Fadhili zake zadumu milele.

11 jNa kuwatoa Israeli katikati yao,

Fadhili zake zadumu milele.

12 kKwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,

Fadhili zake zadumu milele.


13 lKwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.

14 mNa kuwapitisha Israeli katikati yake,

Fadhili zake zadumu milele.

15 nLakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.


16 oKwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,

Fadhili zake zadumu milele.

17 pAmbaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

18 qNaye aliwaua wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

19 rSihoni mfalme wa Waamori,

Fadhili zake zadumu milele.

20 sOgu mfalme wa Bashani,

Fadhili zake zadumu milele.

21 tAkatoa nchi yao kuwa urithi,

Fadhili zake zadumu milele.

22 uUrithi kwa Israeli mtumishi wake,

Fadhili zake zadumu milele.


23 vAliyetukumbuka katika unyonge wetu,

Fadhili zake zadumu milele.

24 wAlituweka huru toka adui zetu,

Fadhili zake zadumu milele.

25 xAmbaye humpa chakula kila kiumbe.

Fadhili zake zadumu milele.


26 yMshukuruni Mungu wa mbinguni,

Fadhili zake zadumu milele.
Copyright information for SwhKC